MSTAHIKI meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa Kata ya Njoro,Zuberi Abdallah Kidumo,ameahidi kugharamia vifaa vya kujifungulia kina mama wajawazito 50 watakaojifungua kwenye Zahanati ya Njoro.
Mbali na hilo,Meya Zuberi Abdallah Kidumo ameahidi kutoa sh milioni moja na nusu kwa familia kumi kutoka kaya maskini wakiwamo yatima kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya.
Ahadi hiyo ameitoa leo
februari 6,2026 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jengo la mama na mtoto
katika Zahanati ya Njoro .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu(wa tatu kutoka kulia)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wodi ya kina mama wajawazito kwenye Zahanati ya Njoro.
Ujenzi wa mradi huo wa wodi ya wazazi katika zahati hiyo ni matunda ya ushawishi kwa Taasisi ya Vijana kwanza uliofanywa na mstahiki meya huyo baada ya kukutana na viongozi wa Taasisi hiyo na kuelezea changamoto zinazowakabili wajawazito wa Kata hiyo wakati wa kujifungua .
Kwa Mujibu wa Meya Zuberi ,Taasisi hiyo ilikubali kufadhili ujenzi wa jengo hilo na kutumia zaidi ya sh,milioni 125.
Meya Kidumo ameomba Manispaa ya Moshi iongeze eneo ili aweze kuongeza wodi nyingine (two in one)na kushauri zahanati ya Njoro iwe Zahanati maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma ya mama na mtoto pamoja na kuwa na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake .
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu,Kidumo amesema kuwa mbali na fedha hizo Taasisi hiyo ilimkabidhi milioni 70 kwa ajili ya kwenda nchi China kununua vifaa kwa ajili ya wodi hiyo .
Amesema Zahanati hiyo itakuwa chachu na itamaliza changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili Wanawake wajawazito kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma ya kujifungua..
Mapema akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa ,mganga mkuu wa Manispaa ya Moshi ,Dtk.Erick Atugonza amesema ujenzi wa Wodi hiyo ya mama wajawazito ulianza mwezi Agosti mwaka 2024 kwa ufadhili wa Taasisi hiyo ya Vijana kwanza likijumuisha chumba cha kujifungulia kina mama,chumba cha uchunguzi wa mawimbi,chumba cha upasuaji( ujenzi wake unaendelea) na kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 125.
Hivi ni moja ya vitanda vya kisasa kabisa ambavyo unavipata kwenye wodi hii ya kina mama wajawazito kwenye zahanati ya Njoro
Amesema vijana kwanza pia wamefadhili vifaa vyenye thamani ya sh,Milioni 160,684,849 ikiwamo vitanda vya wagonjwa,vitanda vya kujingulia,vitanda vya upasuaji ,vifaa vya ufuatiliaji wagonjwa.
Vifaa vingine ni pamoja na kifaa Cha ufuatiliaji wa mjamzito, vifaa vya tiba ya Mwanga wa blue kwa mtoto .taa ya upasuaji ,mashine kuua vidudu,incubator ya mtoto,machela ya dharura.
Zahanari hiyo ya Njoro inahudumia wananchi 12,252 kwa mwaka kutoka ndani na nje ya kata ya Njoro wakiwamo kina mama wajawazito 1,796 kwa mwaka .
“Takwimu hizi zinaonyesha umhimu mkubwa wa zahanati ya Njoro katika kutoa huduma za afya ya msingi kwa jamii inayohudumiwa”,anasema Dkt.Atugonza .
Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi,Zuberi Abdallah Kidumo(aliyesimama)akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa mradi wa wodi ya kina mama wajawazito katika zahanati ya Njoro mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.
.jpg)


.jpg)
.jpg)
.jpg)





.jpg)

.jpg)



0 Comments