HAJI FUNDI HAJI,DIWANI ANAYEYAISHI MAISHA YA WATOTO YATIMA,AJITOSA KUWASOMESHA WENYE UHITAJI KWA MUDA WAKE WOTE WA UDIWANI

 

Diwani wa Kata ya Bondeni Haji Fundi Haji(kulia)akitoa msaada ya vifa vya shule kwa mmoja wa watoto yatima katika hafla fupi ya kuwakabidhi vifaa vya shule watoto hao katika tukio lililofanyika mwaka mpya 2026. 

DIWANI wa Kata ya Bondeni Manispaa ya Moshi ,Haji Fundi Haji ametimiza miaka 32 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1994. 

Lakini akiwa na umri wa miaka sita alimpoteza Baba yake mzazi hivyo kulelewa na mama yake pekee ambaye alisimama kidete pamoja na ndugu na jamaa kuhakikisha Haji anatimiza ndoto ,zake kielimu  na kuanzia hapo alingia kwenye kundi la watoto yatima . 

Haji Fundi Haji ni moja ya watoto yatima waliopitia kwenye mikono ya kituo Cha kulelea watoto yatima na wanaotoka familia duni Cha Bondeni Day Care Orphanance Centre. 

Kituo hiki kilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha watoto hao wanatimiza ndoto zao za kielimu kama anavyoeleza mwenyekiti wa kituo hicho Abbas Kimario . 

Anasema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2002 Lengo likiwa ni watoto yatima wanaishi ndani ya kata ya Bondeni na kazi kubwa iliyofanywa na Taasisi hiyo ni kuwatambua mahali walipo ,mazingira wanayoishi na kubainisha changamoto zao. 

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo lengo jingine ni kufuatilia mienendo ya watoto hao kielimu,kiafya na mazingira wanayoishi na baadae kufanyiakazi changamoto hizo.

"Diwani Haji ni alikuwa miongoni mwa watoto waliolelewa na kituo hiki na sasa anarudisha shukranj kwa kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na yatima vifaa vya shule pamoja na kuwalipia mahitaji mengine ikiwamo ada"anasama. 

Anatoa wito kwa jamii kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwamo kusaidia watoto hao katika mahitaji yao . 

 HAJI FUNDI HAJI HUYO HAPA

Kwa upande wake Diwani anasema msaada anoutoa kwa Watoto hao na makundi mengine si ufahali bali ni Ibaada kwa Imani ya dini yake ya kiislam na pia anasema ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2025-2030,

Anasema anachokifanya kwa sasa kusadia jamii ya waiojiweza wakiwa Watoto yatima si jambo la leo bali ni mwendelezo wa yale ambayo amekuwa akiyafanya kabla hajaingia kwenye siasa.


watoto yatima wakifurahia msosi ulioandaliwa na Taasisi ya Bondeni Day Care Orphanance Centre kwa kushirikiana na Diwani wa kata ya Bondeni Haji Fundi Haji .


“Mimi binafsi nimekwua yatima na nikiwa na miaka sita nilifiwa na baba yangu kuanzia hapo nikalelewa na single mother kwa hiyo najua changamoto za kuwa yatima  hivyo ninachokifanya hapa kwangu mimi si ufahali bali ni ibaada”,anasema .

Anasema mwenyezi mungu akimpa afya njema lengo lake ni kusaidia kila mwaka kwa muda wake wa miaka mitano akiwa mwakirishi wa wananchi kwenye kata hiyo ya Bonden na hadi sasa amesaidia zaid ya Watoto 30 ameneo mbalimbali nchini. 

Haji anasema kila mwaka atahakikisha anasomesha Watoto wapata kumi kwenye vyuo vya kati na vyuo vya mafnzo ya ufundi stadi ikwamo Veta na hadi sasa ameweza kulipia Watoto shule za msingi na sekondari .

Anasema vijana wengi wanashinda mitaani si kwa sababu wamekosa malezi Hapana ni  kutokana na jamii kutotimiza majukumu yake ya kuwasaidia  yao  na kuongeza malengo yao ni kuona Watoto hao wanafanikiwa na wao kama wato misaada wanatimiza malengo yao ya kuwahudumia.

Anasema ni kiu yao kuona Watoto hao wanafanikiwa na kutimiza ndoto zao na kuiasa jamii kuwa sehemu ya mafanikio hayo kwa kutengeneza msingi mzuri wa kuwasaidia



Post a Comment

0 Comments