MAWENZI HOSPITAL YAJIVUNIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

  

 Jengo la Huduma ya Afya ya mama na mtoto kama linavyoonekana . 

HOSPITAL rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi imejivunia uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali kwenye Hospital hiyo ikiwamo kukamilika kwa jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto ambalo hadi kukamilika kwake limegharimu sh,Bilioni 14.617,856,781. 

Jengo hilo linalotoa huduma bora kwa mama wajawazito na watoto na ambalo limekamilika kwa aslimia mia moja na kuwa na  uwezo wa kulaza wagonjwa 150, limekuwa moja ya majengo makubwa na mazuri ambalo limekuwa kivutio kwa wananchi na watu wanaoenda kutembelea jamaa zao. 

Ndani ya jengo hilo zipo wodi binafsi na za kisasa ambazo mgonjwa anaweza kuzitumia kwa gharama nafuu mithiri ya mtu anayeishi Hotel ya kisasa.


Katibu wa NEC -SUKI na mlezi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro,Rabia Abdallah Hamid akiwa kwenye wodi ya kina mama wajawazito kwenye jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto Hospital ya Rufaa ya mkoa Mawenzi . 

Kwa Mujibu wa Taarifa ya mganga mfawidhi wa hospital hiyo (MOI)ambaye pia  ni daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani,Abilahi Issa hospital hiyo kwa sasa inatoa huduma ya wodi binafsi kuanzia daraja la V. I .P,V. V. I.P na EXCUTIVE hii ni kwa ajili ya kuboreshwa huduma na kusogeza huduma  karibu. 

Katika mpango huo serikali imefanikiwa kuokoa mamilioni ya fedha iliyokuwa ikiyatumia kila mwezi kununua mitungi ya Oxygen baada ya kukamilika kwa jengo la hewa tiba ya oxygen lililogharimu Bilioni 1,940,628,011.

 

Daktari Issa alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofanywa na serikali kwenye Hospital hiyo kwa Katibu wa NEC uhusiano wa kimataifa na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa ,Rabia Abdallah Hamid aliyetembelea Hospital hiyo ikiwamo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi(ccm).


Amesema tangu kukamilika kwa jengo hilo na kukabidhiwa kwa uongozi wa Hospital hiyo wameweza kuzalisha mitungi 1,200 na kufanikiwa kuokoa sh,milioni 30 walizokuwa wanatumia kila mwezi kwenda kununua mitungi hiyo sehemu nyingine . 

Kwa Mujibu wa Daktari Issa,hospital ipo kenye hatua za mwisho kuanza ujenzi wa jengo jipya la kisasa(OPD Morden Complex  )kwa wagonjwa wa nje ambalo litakuwa la ghorofa mbili . 

Kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa na manufaa makubwa ikiwamo kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi . 

Pili kutakuwepo na huduma jumuishi zikiwamo za kibingwa pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi,mawenzi kwa  sasa  inao madaktari bingwa 19 huku kukiwa na huduma za kibingwa kumi.

Mawenzi inatekeleza miradi mingine mkubwa ikiwamo ujenzi wa jengo la upasuaji (Surgical Complex )ambalo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu kiasi cha Bilioni 13. 

Mradi mwingine ni jengo kubwa la kuhifadhi maiti ujenzi ambao unatazamiwa kugharimu sh,Bilioni Moja . 

Mawenzi kwa sasa ni miongoni mwa Hospital kumi za rufaa za mikoa ambazo zina CT Scan mbili ambazo ni General CT Scan na Dental Specialized CT Scan ,Digital X -ray mbili na Ultra sound 9. 

Kuhusu utoaji huduma ya uchujaji damu kwa wagonjwa ambao figo zao zimefeli,Daktari Issa amesema kuwa Hospital hiyo inatekeleza maelekezo ya wizara ya afya iliyotoa bei elekezi ya sh,160,000 kwa kila mgonjwa anayehitaji huduma hiyo .

Kwa mgonjwa anayeingia kwenye lango la Hospital hiyo ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,mawenzi anakutana na gengo la wagonjwa wa dharura (Emergency M edicine Department)





Usikose Makala maalumu hivi karibuni juu ya huduma zinazotolewa katika hospital hiyo na miradi iliyotekelezwa na serikali na ambayo ipo kwenye hatua za utekelezaji  hapa hapa kadama24blog

Post a Comment

0 Comments